ALAMA YA MWAMKO MPYA WA WANAWAKE

EmailEmail
عربي Español 
Portugês فارسى
English Deutsch
Bahasa Indonesia Français
Italiano Ceština
Svenska Nederlands
中文 Türkçe
Also available in: Hindi, & Urdu (By E-mail)

KWA NINI NILIVUA “BIKINI” NIKAVAA NIQAB

NA SARA BOKKER

Mimi ni mwanamke mwamerika niliyezaliwa katikati ya nchi.  Nilikuwa kama msichana yeyote nikionyeshwa maisha ya kiduniya katika miji mikubwa mikubwa.  Mwishowe nilihamia Florida na kuenda kuishi Ufuoni wa Kusini.  Huu mtaa unajulikana kwa maisha ya juu.  Kama kawaida nilifanya kama vile msichana yeyote wa kiamerika angelifanya.  Nilielekeza mawazo yangu yote kwa mavazi na urembo.  Nilizingatia utu wangu kulingana na vile watu walivyo nifikiria na maisha ya kisasa.  Nilifanya kazi kwa bidii mpaka nikawa mkufunzi wa mazoezi.  Nilinunua nyumba ufuoni wa bahari.  Ilikuwa kawaida yangu kuonekana nikijionyesha kwenye maskani zilizo ufuoni wa bahari.  Nilijisikia nimetosheka na maisha nikifikiria nimepata maisha niliyotaka.

Miaka ilikuwa imeenda nilipogundua ya kwamba mizani ya kutosheka na maisha na furaha imeaanza kupungua.  Vile nilivyoendelea na kukimbizana na urembo ndivyo nilivyojipata kuwa mtumwa wa mavazi.  Nilikuwa mfungwa wa urembo na mavazi.

Nilizidi kuwa na pengo kubwa baina ya kuridhia na hali ya maisha yangu.  Nilijificha katika starehe, kunywa pombe na kujihusisha na harakati za siasa na hata nilijaribu dini tofauti.  Pengo lililokuwa lidogo lilizidi kupanuka na kuwa bonde.  Mwishowe niligunduwa mambo haya yote yalikuwa hayana uamuzi wa kudumu nilikuwa nikipoza tu.

Baada Septemba 11, nilishuhudia vita vilivyopigwa dini ya Kiislamu, mila na desturi za Kiislamu na utangazaji wa vita vya dini kuhusu uisilamu.  Hapo ndio nilipoaanza kutaka kujua kitu hicho kinachoitwa uisilamu.  Kufikia hapo nilikuwa nikilinganisha uisilamu na wanawake wanaojifunika kwa “mahema”, wanaume wanaowapiga mabibi zao, usharati na ugaidi.

Kama mwanamke anayepigania haki za wanawake na mwana harakati wa siasa ambaye aliyekuwa akitafuta duniya iliyo bora kwa watu wote, njia yangu ilipatana na mwana harakati ambaye alikuwa tayari ameshafika katika uongozi bila ubaguzi, kwa kuendeleza mabadiliko na haki kwa kila mtu.  Nilijiunga na harakati chini ya uongozi wa mshauri wangu mpya.  Harakati zetu kwa wakati huo zilihusu mabadiliko ya kupiga kura na haki za wananchi.  Harakati zangu mpya zilikuwa tofauti, baadala ya kuchagua kupigania  haki watu Fulani, nilijifunza mawazo kama vile haki, uhuru na heshima ni mambo ya kawaida na inafaa kuwa sawa kote duniani.  Pia nilijifunza hakuna tatanishi baina ya uzuri wa mtu na uzuri kwa jumla.  Kwa mara ya kwanza niligundua maana ya watu wote ni sawa.  Lakini jambo  la muhimu nililojifunza ni kwamba inataka imani kuona dunia ni mmoja na kuona usawa  wa viumbe.

Siku mmoja nilipata kitabu ambacho kimechukuliwa kwa ubaya katika nchi za magharibi – Quran Tukufu.  Mara ya kwanza nilivutiwa na mwelekeo na njia za Quran, pia nikapendezwa na lugha yake na mwelekeo wake wa maisha, viumbe na uhusiano wa Muumba na viumbe vyote alivyoumba.  Niligundua Quran inauwezo wa kushauri moyo bila kuhitaji mtafsiri au muhubiri.

Mwishowe nilifikia wakati wa ukweli: Harakati zangu mpya zilikuwa si chochote bila kukubali imani ya kiislamu ambapo nitaweza kuiishi kwa amani kama muisilamu.

Nilinunua nguo nzuri ndefu na kitambaa cha kichwa kama zile zinazovaliwa na wanawake wa kiisilamu.  Nikatembea barabarani na mitaani ambayo siku chache zilizopita  nilikuwa nikitembea na vinyasa, bikini au nguo za mitindo ya kimagharibi.  Ingawaje watu, nyuso na maduka yote yalikuwa sawa, kitu kimoja kilikuwa kimebadilika – sikuwa yule mwanamke wa kitambo.  Moyo wangu ulijaa utulivu na amani nilijisikia mwanamke kwa mara ya kwanza.  Nilijisikia kama nimefunguliwa minyororo niliyokuwa nimefungwa nayo, nilijisikia huru kabisa.  Nilifurahishwa na vile watu walivyoniaangalia na mshangao badala ya vile walivyokuwa wakiniangalia na matamanio kama vile muwindaji anavyo winda mawindo yake.  Nilisikia kama mzigo umetolewa mabegani mwangu.  Sikuwa tena nikimaliza wakati wangu wote nikinunua nguo, nikitumia mapambo ya uso, nikitengenezwa nywele zangu au nikifanya mazoezi.  Mwishowe nilikuwa huru!! Ajabu ni kwamba nilijua uisilamu mahali ambapo  watu wengi   wana pajua kuna fitina nyingi kushinda mahali pengine popote duniani.  Kulingana na hivi mimi huzidi kuwa na upendo na hapa mahali.

Ingawaje nilitosheka na kuvaa hijab nilipendezwa na niqab nilipoona wanawake wengi wa kiisilamu wamevaa.  Nilimuuliza Mume wangu, ambaye tulioana niliposilimu kama ningeweza kuvaa niqab au nitosheke na kuvaa hijab ambayo nilikuwa tayari ninavaa.  Mume wangu alinishauri kwa kuniambia yakuwa yeye anaamini ni wajibu katika uisilamu kwa mwanamke kuvaa hijab lakini si wajibu kuvaa niqab.  Kwa wakati huo hijab yangu ilikuwa ni kitambaa cha kichwa ambacho kilifunika nywele zangu zote isipokuwa uso, na nguo pana nyeusi inayoitwa “Abaya” ambayo hufunika mwili wangu wote kutoka shingoni hadi vidoleni.

Baada ya mwaka mmoja na nusu kupita niliamuambia Mume wangu ya kuwa ningelipenda kuvaa niqab.  Maoni yangu kwa wakati huu ni kuwa nilijisikia ya kuwa nitampendeza Mwenyezi Mungu, Muumba kwa kuzidisha hisia zangu za utulivu na amani kwa kujifunika zaidi.  Alinipa moyo kwa uuamuzi wangu alinipeleka tukaenda kununua “Isdaal” ambayo ni nguo nyeusi pana inayofunika kutoka kichwani hadi vidoleni, na niqab ambayo hufunika kichwa chote na uso isipokuwa macho.

Baadaye habari ziliaanza kuenea kuhusu wanasiasa, wahubiri kutoka Vatican na wanaojiita wapigianaji haki za binaadamu na wana harakati wa kupigania uhuru walipooanza kupinga hijab na niqab.  Kwa wakati mwengine walipinga wakisema yakuwa kuvaa hijab au niqab ni kuwanyanyasa wanawake, pingamizi kwa maendeleo ya muungano wa kijamii.  Hivi majuzi, Ofisa mmoja kutoka Egypt aliita niqab “alama ya kuzorotesha maendeleo”.

Mimi huona ni unafiqi wa serikali za kimagharibi na vikundi vya wanaojiita wapigianaji haki za binaadamu wanapokimbilia kupigania haki za wanawake ingawaje serikali nyengine bado zinaweka vikwazo kuhusu mavazi fulani ya wanawake.  Isipokuwa hawa “wapiganiaji haki” huuangalia kando wakati wanawake wananyimwa haki zao za kufanya kazi au kutafuta elimu kwa maana wamechangua kutumia haki zao kwa kuvaa hijab au niqab.

Leo hii wanawake wanaovaa hijab au niqab wanazidi kunyimwa haki zao kazini na vyuoni vya elimu.  Sio tu katika serikali za kiimla kama vile Tunisia, Morocco na Egypt pia hata demokrasia za kimagharibi kama vile Ufaransa, Uhollandi na Uingereza.

Mpaka leo hii bado mimi hupigania  haki za wanawake, lakini kwa sasa ninapigania haki kama mwanamke wa kiisilamu ambaye anasisitiza mwito wa wanawake wakiisilamu kuchukulia jukumu lao la kuwasaidia waume zao kuwa wanaume bora wakiisilamu.  Kulea watoto wao kwa muongozo ulionyooka wa kiisilamu ili wawe nguzo ya nuru kwa walimwengu wote.  Kukumbushana wema, wema wote na kuzuiia maovu, maovu yote.  Kuzungumza haki na kuzungumzilia juu ya uovu.  Kupigania haki zetu za kuvaa hijab au niqaab na haki zetu kumridhisha Mwenyezi Mungu kulingana na chaguo letu.  Kama vile ni muhimu kuzungumzilia ushuhuda wetu wa kuvaa hijab au niqab kwa wanawake wenzetu ambao hawajapata nafasi ya kuelewa maana yake.  Kwetu sisi kuvaa hijab au niqab huwa tunachukulia moyoni kwa dhati.

Wanawake wengi wanaovaa niqab ni wakimagharibi waliosilimu, wengine wao hata hawajaolewa.  Wengine huvaa niqab bila familia zao au mazingira wanayoiishi kuridhia.  Sisi sote jambo mmoja linalotufananisha ni kuwa tumefanya uaamuzi wa kibinafsi kutokubali kunyanyaswa.

Wanawake hujikuta kwa hiari yao au bila hiari yao katikati ya mitindo ya mavazi kama njia ya mawasiliano kila mahali duniani.  Kama mwanamke wa Kiisilamu, ninazingatia haki za wanawake kwa usawa kujua kuhusu hijab, uzuri wake na amani na furaha inayoleta katika maisha yao kama vile ilivyoleta kwenye maisha yangu.

Jana, bikini ilikuwa alama ya uhuru wangu.  Ukweli wa mambo ni kwamba bikini ilizidi kunipeleka mbali na dini na uzuri wa kuwa mwanadamu mwenye kuheshimika.

Nisingeliweza kufurahi zaidi kwa kuweza kuivua bikini huko Ufuo wa Kusini na maisha ambayo wengi wanafikiria ni ya “kuvutia” ya kimgaharibi ili kuiishi na amani na Mola wangu na kufurahia kuiishi na wanadamu wenzangu kama mtu wa maana.  Hii ndio sababu niliyochagua kuvaa niqab na ndiyo sababu nitakufa nikilinda haki yangu kuivaa.

Leo hii niqab ni alama mpya ya uhuru wa mwanamke kujijua yeye binafsi, sababu yake ni nini na uhusiano ambao atachagua kuwa nao na Muumba wake.

Kwa wanawake wanaofuata kasumba kuhusu nguo ya heshima ya hijab ninawaambia “Hamjuii kile munachokosa”.

Kwenyu nyinyi wafisadi wa maendeleo munaojiita wapiganaji wa vita za kidini ninawaambia “TUENDELEENI”

------------------------------------------------------------

Sara Bokker alikuwa Mcheza Sinema/Modeli/Mkufunzi wa mazoezi na Mwana Harakati.  Kwa sasa yeye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na chama cha “The March for Justice”  Pia ni mmoja wa wawanzilishi na Mtengenezaji  wa Galleria ya bayana iitwayo “Shock & Awe Gallery”
Unaweza kuwasiliana na Sara kwa anwani ya mtandao ifuatayo:
Srae@marchforjustice.com